Saturday, May 11, 2013

JIJI LA DAR ES SALAAM NA AIBU YA UCHAFU,MLIOKO MKOANI HILI NDILO JIJI LETU
Picha juu na chini ni Foleni ya magari ya takataka zaidi ya 30 yaliyokwama katika dampo la Pugu Kinyamwezi kwa takribani siku tatu kutokana na ubovu wa miundo mbinu huku taka zikiendelea kuoza ndani ya magari hayo na kusababisha harufu mbaya kwa wakazi wa maeneo hayo.(Picha na Dewji Blog).
Katapila likiwa katika jitihada za kuchonga barabara ili angalau magari ya taka yaweze kufika eneo la dampo kuwamga taka.
Masela wakifurahia baada ya gari la taka lililokuwa limekwama kufanikiwa kupandisha kilima katika dampo hilo kuelekea kumwaga taka.
Wanafunzi wa shule ya msingi walipokutwa na camera yetu katika dampo hilo wakikatiza na kuzubaa zubaa eneo hilo wakati wa saa za shule.

Wakazi wa maeneo hayo wakichambua takataka hizo kujiokotea chupa tupu za maji na mifuko ya plastiki ikiwa ni ajira waliyojitengenezea katika kuendesha maisha yao ya kila siku, shuhuda wa Mo Blog Zainul Mzige anatanabaisha kwamba chupa wanazookota huuzwa kilo moja kwa shilingi 100 kitu kinachowapelekea wafanyaji wa biashara hii kuwa watumwa wa pombe za kienyeji haswa almaarufu kama Gongo au Chang'aa.
Mitaro ya maji machafu ikiwemo mikojo na vinyesi katika dampo hilo...Je kuna kupona kweli hapa????
Magari ya Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni nayo yalikwama kwenye dampo hilo, pichani yakielekea kuwamga taka hizo baada ya barabara kutengemaa kwa kiasi.
Pichani ni juu na chini Mama lishe wakitoa huduma ya chakula chini ya mti katika eneo lilizongukwa na taka ikiwemo harufu kali na Nzi wanaozunguka hapa na pale lakini vibarua wa dampo hilo hawana la kufanya.
  
Moja ya Katapila lililokodiwa na Halmashauri ya Manispaa ya Dar es Salaam likiwa limekufa na kushindwa kufanya kazi kutokana na kukwamisha na miundo mbinu ya eneo hilo la dampo huku mafundi wakihangaika kulifufua.
Meneja wa Dampo la Pugu Kinyamwezi Bw. Richard Katiti akizungumzia changamoto kubwa wanayokabiliana nayo katika kipindi hiki cha mvua kitu ambacho kinawapelekea kutumia jitihada za ziada ikiwemo kukodisha magari (Vijiko) ili kujitahidi kuhakikisha miundo mbinu ya kufika katika dampo hili inapitika kwa urahisi ili kuondoa vikwazo kwa magari yanayotoa huduma ya kuzoa taka mjini.
Devera wa gari la Kampuni ya usafi ya Green Waste Pro ltd Bw. Ramadhani Sufi akielezea adha wanayoipata ambapo amefafanua kuwa inafika mahali inawabidi kulala siku mbili na gari zenye mzigo wa taka katika mazingira ambayo ndio wanayoshinda na kula kitu ambacho kinaweza kuwasabishia maradhi hivyo ameliomba jiji kurekebisha hali hiyo ili kuwaepusha na mazingira hatarishi kiafya kutokana na uchafu unaolundikana mahali pamoja kuanzia dampo hadi kwenye magari.

Aidha amefafanua kuwa hali hiyo inasababisha kutuchafulia jina la kampuni yetu na kuonekana kama hatufanyi kazi kumbe tatizo lipo kwenye utaratibu mzima wa Manispaa na suala la miundo mbinu.

Pia ameshauri jiji liongezewe uwezo kutokana na kuwa na vyombo vichache na chakavu kitu kinachopelekea kuzidiwa katika kutoa huduma katika dampo hilo.
Mmoja wa madereva wa magari ya taka yaliyokwama kutokana na miundo mbinu mibovu Bw. Frank John akielezea kero ya kwenye dampo la taka lililopo maeneo ya Pugu Kinyamwezi ambapo amesema taka zimelundikana barabara hazipitiki hata magreda ya kuzoa hayana pakupita na kuwaomba watu wanaohusika na dampo kujaribu kutengeneza njia mbadala na kushauri itafutwe njia kipindi cha Masika taka ziwe zinamwaga sehemu nyingine na kipindi cha Kiangazi kiwe na sehemu yake na kushauri mamlaka zinazohusika na usafi zijifunze kutoka kwa wananchi na sisi tujifunze kutoka kwao.

Aidha Bw. John amewataka viongozi wahusika kutokaa maofisini na kutembelea maeneo husika na kujiuliza kwanini gari zinakwama na kuongeza kuwa tatizo hilo limepelekea lawama kwa baadhi kampuni za usafi kushindwa kutekeleza majukumu yake ya kila siku kwa wakati.
Hii ndio hali halisi ya viroba vya uchafu vilivyolundikwa katika eneo la Pugu Kwalala pembezoni mwa barabara na makazi ya watu ambapo wananchi wamekuwa wakizilalamikia kwa sababu kipindi cha mvua vinaweza kuwasababishia magonjwa ya milipuko ikiwemo Kipindupindu.
Mkazi wa eneo la Gongo Mwisho wa lami - Pugu Kwalala Bw.Erasto Njau akilalamikia ubovu wa magari ya taka ya Halmashauri ya Manispaa ya jiji la Dar es Salaam na vile vile utaratibu mbovu wa ukusanyaji wa taka ambapo hata kama gari imeharibika yangetumika magari mengine kuja kubeba taka suala ambalo linalohusu uongozi wa Manispaa ambao ndio unaogharamia magari yanayobeba taka kitu ambacho kinaonyesha utaratibu wa ubebaji taka bado haujakaa sawa.
Mama Lishe Asha Omari Dundo akizungumzia kero ya Mlundikano wa taka katika eneo lake la biashara ambalo sio dampo rasmi la kutupia takataka na anapouliza anaambiwa magari yamekwama dampo kutokana na ubovu wa miundo mbinu kitu ambacho ni hatari kiafya kwa wateja wake wa chakula ambacho ndio biashara anayoifanya kwa ajili ya kusomesha watoto na kila anapouliza hapewi jibu linaloeleweka na ameiomba serikali kutupia macho swala hilo kwa sababu kumekuwa na kauli tofauti malori yamekwama na malori mabovu.
Mama Lishe Asha Omari Dundo akiwaandalia wateja wake chakula cha mchana katika eneo ambalo ni hatarishi kwa walaji.
Mkuu wa Afya Mazingira wa Halmashauri ya manispaa ya Dar es Salaam Bw. Membe Protus Membe akizungumzia jitihada za Manispaa katika kupambana na tatizo la mlundikano wa magari ya taka yaliyokwama katika eneo la Dampo la Pugu Kinyamwezi kutokana na ubovu miundo mbinu ya barabara unaopelekea kukwamisha zoezi la ukusanyaji taka katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar na kusababisha mlundikano wa taka nyingi kwa muda wa kipindi cha siku hizi tatu.

Hata hiyvo amesema katika muda wa siku tatu kuanzia leo Manispaa itahakikisha inarekebisha miundo mbinu ya kuelekea dampo ili kuweza kupunguza msongamano uliopo wa magari ya taka yaliyokwama yaweze kurudi mjini kuendelea na ubebaji wa taka.

Aidha Bw. Membe ameahidi kuwa shughuli za umwagaji taka katika dampo hilo zitakuwa zikifanyika mchana na usiku ili kuondoa mlundikano wa taka mitaani ambao umejitokeza katika muda wa siku tatu.
CREDIT TO dar es salaam yetu & itv

No comments:

Post a Comment